Divock Origi
KLABU ya Fenerbahce ipo kwenye mazungumzo na Liverpool kuhusu kumsajili mshambuliaji, Divock Origi huku Aston Villa, Newcastle, Brighton na Fullham zikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Mirror).

Thiago Alcantara
LIVERPOOL itasubiri mpaka wiki ya mwisho ya dirisha la usajili ili kumsajili rasmi kiungo wa kati wa Bayern Munich, Thiago Alcantara (29). (Talksport).

Jose Gimenez
MANCHESTER City imetoa ofa ya pauni milioni 82 na pauni milioni 4.5 kwa ajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Atletico Madrid Jose Gimenez, 25. (AS).

Lucas Torreira
ARSENAL inaweza kumruhusu, Lucas Torreira (24), kuondoka kwa mkopo kabla ya msimu wa dirisha la usajili kumalizikka, huku Fiorentina na Torino wakiwa wanamtaka kiungo huyo wa kati. (Guardian).

Kalidou Koulibaly
IWAPO Manchester City au Paris St-Germain hawatamaliza mchakato wa kumnyakua, Msenegal Kalidou Koulibaly mpaka mwishoni mwa wiki, Napoli wanatarajiwa kumtoa sokoni mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi (29). (Football Italia).

Sergio Reguilon
MANCHESTER United wapo kwenye mazungumzo na Real Madrid kwa ajili ya Muhispania, Sergio Reguilon. (Marca).

Marcos Acuna
KLABU ya Sevilla, ambayo Reguilon ameutumia msimu uliopita akicheza kwa mkopo, imemsajili beki wa kushoto wa Sporting, Marcos Acuna (28). (Evening Standard).

James Tarkowski
KLABU ya West Ham wanajaribu kumnasa mlinzi wa Uingereza, James Tarkowski (27), baada ya Burnley kukataa ofa ya awali ya pauni milioni 30. (Evening Standard).

Conor Gallagher
KIUNGO wa Chelsea, Conor Gallagher (20), atajiunga na West Bromwich Albion kwa mkopo na anajiandaa kusaini mkataba mpya Stamford Bridge .(Football.London).

Emi Martinez
MLINDA mlango, Emi Martinez (28), anakamilisha mpango wa uhamisho wa thamani ya pauni milioni 20 kwenda Aston Villa baada ya kuchagua kuondoka Arsenal. (Evening Standard)

Bertrand Traore
ASTON Villa ipo mbioni kukamilisha mpango wa kumnasa mshambuliaji, Bertrand Traore (25), kutoka Lyon. (Telegraph).

Alexander Sorloth
KLABU ya Tottenham wanapenda kumsajili mshambuliaji wa Norway, Alexander Sorloth (24), kwa mujibu wa rais wa Trabzonspor Ahmet Agoglu. Sorloth kwa sasa anacheza kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Uturuki akitokea Crystal Palace. (Independent).