CAIRO, Misri
MCHEZAJI tenisi wa Misri, Mayar Sherif, amezungumzia juu ya kazi yake ya kihistoria ya kuwa mwanamke wa kwanza wa Misri kufikia droo kuu ya Roland Garros.


Sherif alikuwa na mechi tatu za kufuzu kabla ya kupata nafasi katika droo kuu, wakati ambapo alimchapa matarajio ya tenisi ya Colombia, Maria Camila Osorio Serrano.
Kisha akaendelea kugonga Caty McNally wa Marikani na Giulia Gatto-Monticone kutoka Italia, wakati hao wote bila ya kupoteza seti moja.


Akizungumza na DMC TV, yoso huyo mwenye umri wa miaka 24 alionyesha kufurahishwa na mafanikio yake na anatarajia kuhamasisha vizazi vya vijana.
“Kwangu imekuwa nzuri. Natumaini kwamba ninachokifanya ni kuhamasisha vizazi vijana. Ninataka wajiamini na watimize malengo yao yote”, alisema.


“Kwangu hii ndio njia muhimu zaidi ya kuchukua kutoka kwa matokeo yangu. Natumai kuwa wasichana wadogo siku zote wanaweza kuweka vichwa juu na kujaribu kufikia malengo yao yote”, aliongeza.
Sherif alimshinda Giulia Gatto-Monticone kwenye michuano ya kila mwaka ya Roland Garros jijini Paris juzi.


Mwanadada huyo alikua mwanamke wa kwanza akiwakilisha Misri kwenye mashindano makubwa ya tenisi (kiwango cha juu) kupatai, baada ya kumchapa Mcolombia, Maria Camila Osorio Serrano.
Aidha, raia huyo wa Misri alimchapa Mmarekani, Katie McNally (6-2, 6-4) kwenye nusu fainali na sasa amefikia rekodi ya kushika nafasi ya 172 duniani.(Goal).