Maendeleo iliyofikia faida kwa ulimwengu

Zanzibar mnufaika, rafiki mkubwa wa China

NA XIE XIAOWU

OKTOBA 1, 1949, Taifa la Jamhuri ya Watu wa China liliundwa.  Zaidi ya miaka 70 sasa, chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) wananchi wa makabila yote na jinsia zote waliungana pamoja kuondosha matatizo yaliyokuwa yakiwakabili ndani na nje ya China.

Hatimaye walifanikiwa kuwa taifa bora na lenye mafanikio, pamoja na kuchangia mafanikio katika sehemu kubwa ya dunia ikiwa ni kuimarisha amani pamoja na mshikamano.

Zaidi ya miaka 70 sasa, zaidi katika miongo minne iliyopita mabadiliko makubwa yametokea China chini ya uongozi wa CPC, wananchi wa China wameungana na kuonyesha maajabu makubwa katika maendeleo ikiwa imeweka historia ya dunia.

Imeamua kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea yenye tabia na kukubalika na China, imefungua milango ya mabadiliko, ikitilia mkazo sio tu maendeleo ya uchumi pekee bali pia kutilia mkazo zaidi ustawi wa wananchi wa China. Dhana ya ‘watu kwanza’ ndio chachu ya mabadiliko ya China.

China sasa imekuwa nchi ya pili kwa uchumi bora duniani.  Pato la Taifa (GDP) limekuwa kutoka USD 35 mwaka 1949 hadi USD 10,000 mwaka 2019. 

Cha umuhimu cha chenye kutia moyo zaidi ni kwamba zaidi ya wananchi wa China 1.4 billion wataondokana na umasikini na umasikini uliokithiri mwishoni mwa mwaka huu.

Haya ni mafanikio makubwa ya mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea wenye tabia na kukubalika na China.  Haya ndio mafanikio makubwa ya muendelezo wa haki za Binaadamu na maendeleo ya wananchi duniani. 

China inajivunia mafanikio makubwa katika maendeleo yake, kufanya kazi kwa bidii, busara pamoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wa China.  Uimara wa China pia umechangia amani na utulivu wa dunia kwa kuweka mazingira bora ya ushirikiano wa kimataifa kwa kuhimiza na kuimarisha mashirikiano katika sehemu kubwa ya dunia.  Mafanikio ya China sio tu yamefanikiwa kuwanufaisha wananchi wa China pekee bali pia sehemu kubwa ya dunia.

China mara zote imejikita kutoingilia masuala ya ndani ya nchi yoyote duniani, zaidi ni kukuza ushirikiano na mashirikiano kimataifa.  Mara zote China imekuwa mchangiaji mkubwa katika kulinda na kudumisha amani ya dunia, ushirikiano katika kutenda haki na imekuwa ikipambana na aina zote za udhalilishaji, unyonyaji na ukandamizaji katika mataifa ya dunia. 

Katika kufanikisha hayo, China imekuwa taifa la pili kwa ukubwa duniani kuchangia katika Umoja wa Mataifa (UN) katika masuala ya ulinzi wa amani ikichangia kwa kiasi kikubwa walinda amani katika sehemu mbali mbali za dunia na pia kuwa mwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN Security Council).

China ni mchangiaji mkubwa katika sekta ya maendeleo ya dunia, imekuwa ikiongoza kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia.  Kwa karibu miongo minne iliyopita tokea kufanyika kwa mabadiliko makubwa ya kiuchumi, uchumi wa china umekuwa ukikua kwa kasi sana kulinganisha na matifa mengine mengi makubwa duniani.

Kwa zaidi ya miaka 10 sasa China imekuwa ikichangia ukuaji wa uchumi wa dunia kwa zaidi ya asilimia 30 na zaidi ya asilimia 70 katika mapambano ya kupambana na umasikini duniani.

Miezi michache iliyopita wakati wa janga la mapambano dhidi ya Corona (COVID-19) China ilizindia kampeni kubwa ya dunia ya misaada ya kibinaadamu, ikiwa ni ya kiwango kikubwa katika historia ya Jamhuri ya Watu wa China.

China imefanikiwa kutoa msaada wa madawa kwa zaidi ya nchi 150 duniani pamoja na kuitikia wito wa jumua za kimataifa juu ya umuhimu wa misaada ya dharura katika kipindi cha mapambano hayo.

China imekuwa ikitoa mafunzo kwa kupitia mtandao (video conferences), baina ya wataalamu wa afya wa China na wenzao katika zaidi ya nchi 180 za dunia; wakibadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya jinsi ya kupambana na ugonjwa wa COVID-19 pamoja na magonjwa mengine bila ya kuathiri ustawi wa jamii wan chi husika.

Katika kipindi hicho, china imefanikiwa kutoa vikundi 33 vya wataalamu katika nchi 31 za dunia kutoa mafunzo ya moja kwa moja ikiwa ni jitihada za kupambana na ugonjwa huo.

Vikundi vya wataalamu bingwa na wabobezi wamo katika harakati za makusudi za kutafuta kinga na tiba za ugonjwa huo na pindi ikipatikana itakuwa ni faraja kwa china ambayo itaweza kuisambaza tiba hiyo katika sehemu kubwa ya dunia kwa lengo la kukuza ustawi wa wananchi duniani na hasa katika nchi zinazoendelea.

Mkwamo wa dunia uliosababishwa na COVID-19, pamoja na changamoto nyingi nyengine, zinaiingiza China na dunia katika awamu mpya. 

China pamoja na kuungana na dunia katika mapambano dhidi ya COVID-19, inaimarisha juhudi zake katika kuimarisha uchumi-jamii, wenye lengo la kuimarisha na kuanzisha mfumo mpya wa mashirikiano kitaifa na kimataifa bila ya kuwepo mvutano baina ya wahusika.

Pato la Taifa (GDP) katika robo ya pili ya mwaka limeongezeka kwa asilimia 3.2, ikiiweka China katika ramani ya kuwa nchi ya kwanza duniani ambayo uchumi wake umeimarika kwa kasi tokea kupungua kasi ya COVID-19. 

Hatua hii inazidi kuifanya China kuwa nchi kinara duniani katika uimarishaji wa uchumi licha ya misukosuko mbali mbali inayoendelea kuikabili dunia.  Hali hii inaonyesha uimara zaidi wa uchumi wa China.

China kamwe haiwezi kuisahau Afrika katika juhudi zake za pamoja za mashirikiano ikiwemo ya uimarishaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla. Ushirikiano na hatua Afrika na China zinazopita zimekuwa zikifanana na daima zimekuwa katika mashirikiano ya pamoja.

Katika kikao cha pamoja cha mashirikiano baina ya China na Afrika (Beijing Summit of China-Africa Cooperation Forum, 2018), Rais wa China Xi Jinping alihamasisha ushirikiano baina ya China na Afrika kwaajili ya maisha bora ya baadae kwa wananchi wa pande husika.  Awamu mpya ya mashirikiano baina ya Afrika na China ilizinduliwa.

Urafiki na uhusiano kati ya China na Tanzania ni wa muda mrefu sana na wenye historia iliyotukuka.  Ushirikiano na urafiki kati ya China na Zanzibar una umuhimu mkubwa katika kujenga mahusiano na kudumisha urafiki kati ya China na Tanzania.

China ilikuwa ni miongoni mwa nchi za mwanzo duniani kuytambua Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.  Tokea mwaka huo vikundi vya wataalamu wa afya na madaktari bingwa wamekuwa wakifanya kazi Zanzibar.

Wataalamu na mfundi mbali mbali kutoka China wamekuwa wakifanya kazi Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo.

Mathalan, kundi la wataalamu wamekuwa wakifanya kazi ya kuimarisha mitambo ya redio na televisheni kwa lengo la kuwapatia wananchi wa Zanzibar huduma bora za matangazo na vipindi kupitia Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Mikataba mbali mbali ya mashirikiano na mahusiano imefungwa kati ya China na Zanzibar na China na Tanzania kwa lengo la kudumisha mashirikiano baina ya nchi hizi ambayo imekuwa na faia kubwa kwa Zanzibar na Tanzania. Hii ni kuonyesha wazi kuwa China ni rafiki na mshirika mwenza katika maendeleo ya Zanzibar na Tanzania.

Katika miaka ya hivi karibuni China imehamasisha misaada katika miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali, zahanati na vituo vya afya, ujenzi wa shule katika viwango tofauti, huduma za taa za barabarani pamoja na usambazaji wa maji safi na salama.

China pia imetoa nafasi za ufadhili wa masomo kwa viwango tofauti nchini ikiwemo mafunzo ya muda mfupi na mafunzo ya muda mrefu.

XIE XIAOWU.

Mradi wa Serikali Mtandao (e-Government) pamoja na ukamilishwaji wa Uwanja wa ndege (Terminal III) utachangia zaidi maendeleo ya zanzibar hasa katika sekta ya utalii ambayo imekuwa ni miongoni mwa sekta muhimu katika uimarishaji uchumi wa Zanzibar.

Wananchi wa Zanzibar na Tanzania wamehamasika na misaada na mashirikiano na China; ikithibitika kwa madarasa mbali mbali ya lugha ya Kichina (Confucious Class) kuzidi kuwa maarufu nchini.

Katika kipindi cha mapambano dhidi ya COVID-19, China imekuwa karibu sana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweza kuwapatia misaada mbali mbali ikiwemo ya vifaa-tiba na mingine ya kijamii kwa mashirikiano ya pamoja kwa kutambua mahitaji ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania katika kipindi kigumu cha mapambano hayo.

China itaendelea kuisaidia Zanzibar katika mipango yake mbali mbali ikiwemo ya uchumi na ustawi wa jamii kwa lengo la kukuza mashirikiano ya muda mrefu ambayo China na Zanzibar imedumu nayo.

Xie Xiaowu

Balozi mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China, Zanzibar.