NA ABDI SULEIMAN

CHAMA cha Alliance For Democratic Change (ADC), kimelaani vikali kauli zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa, ambazo zinaashiria uvunjifu wa amani nchini.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ADC Taifa, Omar Costantino Pweza, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya kanda ya ADC Wawi.

Hata hivyo alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua kwaniADC haiko tayari kuona wananchi wanafanya vurugu kwa sababu ya siasa.

Aliwataka vijana kujitambua na kuheshimu amani, umoja na mshikamano uliopo.Aliwaomba viongozi wa vyama vya siasa, kufanya kampeni na kuomba kura kwa amani, kwani Tanzania inahitaji amani.