BLOEMFONTEIN,AFRIKA KUSINI

IDADI  ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya Corona nchini Afrika Kusini imefikia 630,595, huku idadi ya vifo ikifikia 14,389.

Waziri wa afya wa nchi hiyo Zweli Mkhize alisema,hivi sasa idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona waliopona nchini humo imefikia 553,456, kiwango ambacho kimefikia asilimia 87.

Kadiri hali ya maambukizi ya virusi vya Corona inavyopungua, ndivyo uchumi wa nchi hiyo unavyopiga hatua ya kufufuka.

Hivi karibuni, waziri wa utalii wa Afrika Kusini Mmamoloko Kubayi-Ngubane alisema, ingawa ndani ya muda mfupi, hatua za kuhimiza utalii wa ndani zitadumishwa na kuwa kipaumbele katika utalii nchini humo, lakini katika kipindi kijacho utalii wa kimataifa utafunguliwa tena.

Mbali na hayo viwanja vya michezo, mambo ya kujenga afya, na sekta ya utengenezaji wa mvinyo ambazo ziliathiriwa vibaya na janga hilo vilevile zilirejeshwa kwenye hali ya kawaida hatua kwa hatua.