NA MARYAM HASSAN
MKAAZI wa Tunduni amepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana aliyopewa katika mahakama ya mkoa Mwera.
Mshitakiwa huyo ni Mohamed Wiliam Kurwa (28) ambae alitakiwa kusaini bondi ya shilingi 500,000 pamoja na kuwasilisha wadhamini wawili ambao watasaini kima hicho hicho.
Pia wadhamini hao wametakiwa kuwasilisha kopi ya kitambulisho cha Mzanzibar mkaazi bamoja na barua ya Sheha wa shehiya wanayoishi.
Masharti hayo yametolewa na Hakimu wa mahakama ya mkoa Mwera Said Hemed Khalfan, na kueleza kuwa endapo mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana hadi Septemba 28 mwaka huu, lakini masharti ambayo yamemshida.
Mshitakiwa huyo alifkishwa mahakamani hapo kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya, kosa hilo anadaiwa kutenda Septemba 17 mwaka jana.
Kosa hilo anadaiwa kupatikana nalo majira ya saa 2:00 za usiku huko Mwera skuli akiwa na kete 54 zikiwa kwenye kifuko chenye kuonesha ambazo zinasadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.
Ilidaiwa kuwa dawa hizo ni aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 0.909 kitendo ambacho ni kosa kisheria.