NA TATU MAKAME
KIJANA Ali Omar Ali (23) mkaazi wa Mfenesini Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja, anaekabiliwa na kosa la kumtorosha mtoto aliyechini ya uangalizi wa wazazi wake anatarajiwa kufikishwa tena katika Mahakama ya Mkoa Vuga Unguja Septemba 7 mwaka huu.
Mshitakiwa huyo alitenda kosa kwa kumtorosha mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) kwa kumchukua nyumbani kwao na kumpeleka nyumbani kwao ndani ya chumba, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 113 (1) (a) cha sheria namba 6 ya mwaka 2018.
Imeelezwa Februari 12 mwaka huu majira ya saa 7:00 za mchana mshitakiwa huyo alimtorosha mtoto huyo, na kumpeleleka chumbani kwake ndani ya nyumba yao bila idhini ya wazazi na siku hiyo hiyo saa 2:00 usiku alimuingilia kimwili jambo ambalo ni kosa kisheria.
Kosa hilo likiwa ni kinyume na sheria chini ya kifungu cha 108 (1) (2) na kifungu cha 109 (1) sheria namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar .
Hata hivyo mshitakiwa huyo yupo rumande hadi Septemba 7 kesi yake itakaposikilizwa tena mahakamani hapo.