NA MARYAM SALUM, PEMBA

Shaaban Ali Shaaban, “Shaaban Mapinduzi” 28 mkaazi wa Pujini Wilaya ya Chake Chake, ametinga katika Mahakama ya Mkoa kujibu shitaka lake, baada ya kupatikana na tuhuma za kumbaka mtoto wa kike mwenye miaka 15.

Wakati akisomewa shitaka lake na Mwendesha Mashitaka, Mohamed Ali Juma, mtuhumiwa alikataa, ambapo Mwendesha Mashitaka huyo, aliiomba mahakama husika iahirishe shauri na ipange tarehe nyengine kwa vile

mtuhumiwa amekataa.

“Muheshimiwa kwa vile mtuhumiwa amkekataa shitaka lake, hivyo tunaiomba Mahakama yako iahirishe shauri na ipange tarehe nyengine tuweze kuita mashahidi kwa ajili ya kusikilizwa,”alidai Mwendesha

mashitaka.

Mwendesha Mashitaka, alidai  tarehe isiyofahamika Januari mwaka huu,mtuhumiwa alipatikana na kosa la kumbaka mtoto wa kike mwenye miaka 15, ambaye yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake.

Wakati Mwendesha Mashitaka akimsomea mtuhumiwa kosa lake linalomkabilimbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Luciano Makoye Nyengo, alidai kuwa kitendo hicho kilifanyika Januari, saa 7:00 mchana shehia ya Pujini

wilaya ya Chake Chake , ambapo siku na tarehe haikufahamika. Baada ya ombi la upande wa mwendesha mashitaka, Hakimu Luciano hakupingana nalo na shauri liliahirishwa hadi Septemba 22 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa, pia indhari kwa  mashahidi waweze kuhudhuria.