ZASPOTI
KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amesifu nguvu ya akili ya timu yake baada ya Eddie Nketiah, kufunga goli la uishindi na kudumisha mwanzo wao wa asilimia 100% msimu dhidi ya West Ham.
Matokeo hayo yaliwafanya ‘wagonga nyundo’ kujikuta wakiambulia kipigo cha pili mfululizo, mara ya tatu katika misimu minne iliyopita wamepoteza mechi zao mbili za kwanza.
“Ninachokipenda ni njia ambayo vijana walikuwa nayo katika dakika 25 za mwisho ambapo niliona walikuwa chini kidogo na kisha wanapanda”, alisema, Arteta.
“Labda miezi michache iliyopita tungetoka sare au kupoteza mchezo huo na leo tunaushinda. Mwishowe lazima utafute njia kwa sababu kutakuwa na michezo kama hii msimu huu.”
Washika bunduki walidhibiti kwa kiwango kikubwa hatua za ufunguzi wa mchezo na walistahili kuendelea wakati Alexandre Lacazette alipojitwika krosi ya Pierre-Emerick Aubameyang na kuandika goli la kwanza kunako dakika ya 25.
Hata hivyo, wagonga nyundo, ambao kila wakati walionekana kuwa hatari kwenye shambulio la kushtukiza, walisawazisha kabla kipindi cha kwanza kumalizika wakati Michail Antonio alipofunga krosi ya Ryan Fredericks.
Lakini, Nketiah akafunga goli la ushindi dakika ya 85 kutokana na Dani Ceballos kuihakikisha Arsenal inaendeleza rekodi yao nzuri ya nyumbani dhidi ya wagonga nyundo, baada ya kushinda michezo 11 kati ya 12 ya mwisho kwenye uwanja wa Emirates.
Katika mchezo mwengine, Manchester United ilianza vibaya msimu wa Ligi Kuu ya England, baada ya kutandikwa magoli 3-1 na Crystal Palace kwenye uwanja wa Old Trafford.
Mshambuliaji wa Ivory Coast, Wilfried Zaha, alifunga mara mbili dhidi ya klabu yake ya zamani akimuacha kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer kinywa wazi.
Zaha aliana
Winga, Andros Townsend, alifunga goli la kuongoza kunako dakika ya saba kufuatia krosi iliyochongwa na Jeffrey Schlupp kabla ya Zaha kuongeza la pili kunako dakika ya 74 kwa mkwaju wa penalti.
Mwamuzi, Martin Atkinson alitumia ‘VAR’ kuamua iwapo Victor Lindelof, aliunawa mpira ndani ya sanduku lake mwenyewe. Lakini, baada ya David de Gea kuokoa mkwaju wa Jordan Ayew, Atkinson aliamuru kurudiwa kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania alikuwa amehama mstari wake. Zaha alichukua jukumu la jaribio la pili na hakukosea.
Akicheza mechi yake ya kwanza, Donny van de Beek, aliifungia goli la kufutia machozi United huku Zaha akikamilisha karamu hiyo ya magoli dhidi ya klabu yake ya zamani.
Ulikuwa ushindi wao mkubwa kabisa huko Old Trafford, mara ya kwanza kuifunga United ugenini na nyumbani katika misimu mfululizo na inamaanisha Palace imeshinda michezo yao miwili ya ufunguzi wa msimu wa ligi hiyo ya juu kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Matokeo mengine ya ligi hiyo, Everton iliilaza West Brom magoli 5-2 na Leeds ikaitandika Fulham 4-3.(BBC Sports).