LONDON, England

MIKEL Arteta, kocha mkuu wa Arsenal amesema mshambuliaji wake namba moja Pierre Emerick Aubameyang atasaini mkataba mpya hivi karibuni.

Arteta ameongoza kikosi chake kutwaa mataji mawili kwa kuzinyoosha timu kubwa ikiwa ni pamoja na ule wa Kombe la FA ,ambapo aliichapa Chelsea mabao 2-1 na taji la Ngao ya Jamii alishinda kwa penalti 5-4 mbele ya Liverpool baada ya dakika 90 kutoka sare ya bao 1-1.

Mtupiaji wa mabao yote matatu alikuwa ni nahodha Aubameyang ambaye amekuwa akitajwa kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Arteta amesema:”Nimekuwa nikisema jambo lilelile kuhusu Aubameyang. Ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kucheza michezo mikubwa.

“Nimekuwa nikipambana kuhakikisha namshawishi ili aweze kubaki kwenye timu hii naamini kuwa atakubali kusaini kwa kuwa hii ni timu yake bora na tukiwa pamoja tutafanya makubwa msimu ujao,”.

Msimu mpya wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuanza Septemba 12 na mabingwa watetezi ni Liverpool.