KIGALI,RWANDA

SERIKALI imeweka mpango wa kufufua uchumi kama moja ya mikakati ya kufufua uchumi kwa kuzingatia ulinzi wa jamii, ikitoa msingi mzuri kwa wanyarwanda walio katika mazingira magumu kuanza kujenga maisha yao.

Taarifa zinaeleza kuwa asasi za kiraia zinazozingatia wanawake, juu ya athari ya Covid-19, zinaonyesha kwamba maisha ya wanawake kiuchumi na uzalishaji yaliathiriwa tofauti na wanaume.

Athari za kijinsia za Covid-19 na hatua zinazoambatana za kuzuiliwa zinazotambuliwa na mashirika zinazingatia unyanyasaji wa kijinsia (GBV), elimu ya wasichana, ufikiaji wa wanawake wa fedha, na sauti ya wanawake na ushiriki katika misaada na urejesho.

Mratibu wa Kitengo cha Utekelezaji wa Miradi katika Wizara ya Jinsia na Ukuzaji wa Familia Alex Twahirwa, alibainisha kuwa janga hilo linatishia kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana juu ya usawa wa kijinsia na kuzidisha umaskini.

Wanachama walipendekeza kuwa fursa za ufadhili zijumuishwe zaidi kwa wanawake kama vile vigezo vya uteuzi kutoa haki kwa wanawake, ambazo zilisemwa katika taarifa ya pamoja juu ya athari za kijinsia za Covid-19.

Alisema biashara zinazomilikiwa na wasichana zimeathirika zaidi, kwani walipoteza mitaji yao yote kwa sababu asilimia 74 ya wanawake wako katika sekta isiyo rasmi ya biashara.

Alisema mipango ya kufufua uchumi na ujumuishaji kijamii na bajeti inapaswa kushughulikia changamoto za wanawake,wasichana na kutoa mifumo, nafasi zisizoathiri mchakato wa kufufua uchumi katika ngazi zote,”alisema.

Mchumi Mkuu katika Wizara ya Fedha na Mipango ya Uchumi Amina Umulisa Rwakunda, alisema kuwa wizara hiyo inachambua sekta ambazo zinaathiriwa zaidi na janga hilo na jinsi zinavyoweza kuungwa mkono kwa kuwapa misaada ya ushuru kwa ushuru maalumu.

Haguruka, alirikodi ongezeko la asilimia 75 ya visa vilivyoripotiwa vya GBV kuhusiana na kesi zilizorikodiwa hapo awali.

Vizuizi vya kukaa nyumbani na hatua nyengine ambazo zilizuia harakati za watu zilichangia kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Wanawake na wasichana ambao tayari wako katika hali za unyanyasaji walikuwa wazi zaidi kwa udhibiti na vizuizi na wale wanaowanyanyasa, hakuna njia ya kutafuta msaada.

Matokeo zaidi kutoka kwa Oxfam- Rwanda yanaeleza  kuwa kuzuiliwa kulizidisha udhaifu kwa waathiriwa wa GBV,haswa vijana.