NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KIKOSI Cha timu ya Azam FC, kinatarajiwa kuondoka leo mchana kwa basi kuelekea Mkoani Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City.

Katika mchezo uliopita Azam walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union wakiwa katika Uwanja wao wa nyumbani Azam Complex, uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Huku Mbeya City wakiwa wametoka kupoteza dhidi ya Yanga bao 1-0 mchezo uliopigwa kwenye dimba la Mkapa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumapili, Septemba 20 katika Uwanja wa Sokoine mkoani humo.

Akizungumza na Zanzibar Leo jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo Zakaria Thabit, alisema  timu imeondoka leo kuelekea Mbeya kwenye mchezo wao watatu wa ligi.

Alisema kikosi hicho kina watu  35 ambao ni viongozi, benchi la ufundi na wachezaji 23.

“Tunakwenda kuvana na Mbeya City ushindi ndio mipango yetu na tumeondoka na kikosi cha jumla ya watu 35 wakiwamo viongozi.

“Baada ya hapo, Septemba 21 tutaenda Sumbawanga kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons,  Septemba 26,” alisema