NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

BEKI wa timu ya Yanga SC, Lamine Moro ameahidi timu yao kuendelea kufanya vizuri baada ya kuungana vizuri.

Lamine juzi aliipatia timu yake bao la ushindi dhidi ya Mbeya City katika mchezo wao uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Akizungumza baada ya mchezo huo Moro alisema wanamahukuru Mwenyezi Mungu kwa ushindi walio upata na timu ikiunganika vizuri watazidi kupata matokeo mazuri

Alisema wana imani mbele watakuwa wazuri zaidi lakini kubwa amefurahi kuwa sehemu ya ushindi ambao umepatikana juzi kwenye dakika za majeruhi.

“ Namshukuru Mungu kwa kweli tumepata ushindi wa bao moja mchezo ulikuwa mzuri wapinzani wetu walikuwa vizuri sana kama sisi , “ alisema