NA ZAINAB ATUPAE
TIMU ya Bondeni FC imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tolla Combine,ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya Coco Sport hatua ya mtoano.
Mchezo huo uliopigwa majira ya saa 10:00 jioni ambao ulikuwa na mashabiki wengi.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko hakuna aliyefanikiwa kuliona lango mwenzake.
Kurudi kumalizia kipindi cha pili wanaume hao waliingia kwa kasi kubwa,huku kila mmoja kufanya mabadiliko ya kurekebisha kikosi chake kwa ajili ya kupata bao.
Lakini dakika ya 79 Salim Bajaka aliweka bao na kudumu hadi mwisho wa mchezo huo.
Ruiz Yussuf wa timu ya Bondeni FC alifanikiwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kupatiwa zawadi ya fulana.