NA HANIFA SALIM

WANANCHI wametakiwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kiweze kuendelea kuongoza nchi.

Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba, Yussuf Ali Juma, wakati akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa kampeni za wagombea wa CCM jimbo la Chake- Chake, katika kiwanja cha Tibirinzi.

Alisema, CCM ina kila sababu ya kubakia madarakani na kuongoza nchi kutokana na maendeleo makubwa iliyofanya katika kipindi cha miaka mitano.

Mgombea wa uwakilishi jimbo hilo, Shaibu Hassan Kaduara alisema, ana imani thabiti ya wananchi wa jimbo hilo na kuahidi endapo atapata ridhaa ya kuongoza atajenga barabara za ndani za mji huo ikiwemo ya Misooni, Gongomawe, Shamiani, Minazini na Ngomahazingwa.

Katika ufunguzi wa kampeni hizo jumla ya wanachama wapya 110 walikabidhiwa kadi za CCM.