PARIS, Ufaransa
KIUNGO, Cesc Fabregas amefikisha mechi 800 tangu aanze kucheza soka la kulipwa mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 16 alipojiunga na Arsenal.

Lakini rekodi hiyo ameiweka akiwa na timu ya Monaco ambapo idadi hiyo ya mechi inahusisha ngazi ya klabu na timu ya Taifa.

Fabregas zao la akademia ya Barcelona akiwa pamoja na Lionel Messi ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa, akicheza kwenye nafasi ya kiungo mshambuliaji.

Pamoja na ushindani alioukuta kwenye timu ya Arsenal katika nafasi yake hasa alipokuwepo, Patrick Viera, ilimchukua muda mchache kupata nafasi na kuwa mchezaji muhimu Emirates.(Goal).