BEIJING,CHINA

CHINA inakumbuka  miaka 75 tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia katika bahari ya Pasifiki, ambapo nchi hiyo ilikumbana na uvamizi wa kinyama na kukaliwa kwa sehemu kubwa ya ardhi ya nchi hiyo na Japan.

Kiongozi wa chama tawala cha Kikomunist na mkuu wa taifa hilo Xi Jinping aliwaongoza maofisa wa Serikali kukaa kimya kwa dakika moja pamoja na kuweka mashada ya maua katika ukumbi wa kumbukumbu kwa heshima ya wanajeshi na raia ambao walishiriki katika mapambano.

Japan iliivamia China mwaka 1937, huku kukiwa na vita katika miji na matukio mabaya kama ubakaji.

Licha ya kuwa Japan ilisalimu amri rasmi katika meli ya kivita ya USS Missouri Septemba 2, 1945, China inaadhimisha mwisho wa vita hivyo Septemba 3, wakati ilipofanya sherehe za nchi nzima.