BEIJING, CHINA

CHINA imesema kuwa inafanya mazoezi ya kijeshi karibu na mlango wa bahari wa Taiwan ili kulinda mamlaka yake wakati maofisa wa ngazi za juu kutoka Marekani wakiwa ziarani nchini Taiwan.

Mazoezi ya kijeshi yanafanyika wakati kukiwa na mvutano mkubwa kati ya Beijing na Washington na wakati Marekani ikiahidi kukipatia msaada kisiwa hicho ambacho China inasema kiko kwenye milki yake.

Keith Krach ni ofisa wa juu kutoka Wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuzuru kisiwa hicho kwa miongo kadhaa.

Hapo jana msemaji wa wizara ya ulinzi nchini China, Ren Guoqiang ameishutumu Marekani na Taiwan kwa ushirika wao wenye hila na kusababisha migongano, ingawa hakuzungumzia ziara hiyo.

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuitumia Taiwan kuidhibiti China au kutegemea nchi za kigeni kujiimariha ni mawazo ya kufikirika.

Guoqiang alisema mazoezi ya kijeshi katika eneo hilo ni halali na muhimu kwa eneo la bara kwa ajili ya kulinda himaya na uaminifu ”, alisema.

Krach, ambaye, yuko chini ya Waziri wa Marekani anayeshughulikia masuala ya uchumi, atakutana na rais wa Taiwan Tsai Ing-wen baadae Ijumaa.

Ingawa Marekani haina mahusiano rasmi ya kidiplomasia na Taiwan, sheria ya mahusiano ya mwaka 1978 inaruhusu Marekani kuuza silaha kwenye kisiwa hicho, na kufanya kuwa mahusiano ya karibu.