COLOMBO, SRI LANKA  

ZAIDI ya wanafunzi 700 kutoka skuli 19 katika mji mkuu wa Sri Lanka wamepokea zawadi za vifaa vya kuandikia na mifuko ya panda kutoka ubalozi wa China nchini Sri Lanka.

Taarifa zilisema kuwa wanafunzi waliopata msaada huo ni kutoka jamii tofauti za kidini ambao walionesha furaha wakati wakikabidhiwa zawadi hizo katika hafla iliyofanyika katika kitongoji kimoja mjini Colombo.

Kutokana na miongozo ya afya, serikali ya Sri Lanka kwa sasa inakabiliana na janga la COVID-19, ambapo ni wanafunzi 100 tu na walimu wao waliruhusiwa kukusanyika katika ukumbi wa skuli ya Al Hidaya.

Waandaaji  walisema wanafunzi waliochaguliwa kupokea zawadi hizo walikuwa wanafunzi wa darasa la 10 ambapo vifaa walivyokabidhiwa kuwa ni pamoja na vifaa vya kuandikia na mikoba.

Kupewa zawadi kwa wanafunzi hao ni uhusiano uliopo kati ya China na Sri Lanka ambapo ubalozi wa China una upendo na mapenzi kutoka kwa watu wa China.

Hu Wei, ambae ni balozi wa China nchini Sri Lanka, alikabidhi zawadi hizo kwa wanafunzi na kuwataka wasome kwa bidii.

“Natumai kuwa wanafunzi watasoma kwa bidii, watakua wakakamavu, na watajiunga na urafiki na ushirikiano wa kiutendaji kati ya China na Sri Lanka huku wakitoa michango yao wenyewe kwa maendeleo ya nchi,” Hu alisema.