UBALOZI wa China nchini Sudan Kusini umetoa tani 3,000 za mchele kama msaada wa dharura kwa taifa hilo ambalo linakabiliwa na tishio la uhaba wa chakula.

Waziri wa mambo ya kibinadamu wa Sudan Kusini, Peter Mayen Majongdit ameishukuru China kwa msaada wa mchele kwa niaba ya wananchi wa Sudan Kusini.

Majongdit aliongeza kuwa, uhusiano kati ya Sudan Kusini na China ni mzuri na nchi hizo mbili zitaimarisha uhusiano huo kwenye sekta mbalimbali.