BEIJING,CHINA
CHINA imevishutumu vikosi vya jeshi la India kwa kukiuka makubaliano ya pamoja na kufyatua risasi za tahadhari hewani katika makabiliano na wafanyakazi wa China mpakani.Hayo yanajiri huku kukiwa na hali mpya ya wasi wasi kati ya nchi hizo mbili.
Walinzi wa mpaka wa China walichukua hatua za kulipiza kisasi kutuliza hali, Zhang Shuili, msemaji wa kamandi ya magharibi ya jeshi la nchi hiyo, alisema katika taarifa iliyochapishwa na tovuti rasmi ya jeshi.
Taarifa hiyo haikuweka wazi hatua hizo iwapo wanajeshi wa china pia walifyatua risasi za tahadhari. Pande zote mbili zinatumia utaratibu wa muda mrefu uliopo wa kuepuka kutumia silaha katika mpaka wao huo ulioko milimani unaopitia katika milima ya Himalaya, licha ya kuwa makubaliano haya hayajazuwia makabiliano ambayo yalisababisha maafa.