MNAMO mwezi Agosti mwaka 2020 kuliripotiwa kupanda maadufu kwa bei ya dhahabu ambapo gramu 28 thamani yake ilikuwa zaidi ya pauni 1,575 ya juu ya dola 2,000.

Wakati bei hii ilitokana na wafanyabiashara wa dhahabu, kulizuka swali la usambaaji wa madini hayo adimu na ni lini hasa yatakuwa hayapatikani tena duniani.

Dhahabu ni madini ambayo uhitaji wake ni wa juu sana katika uwekezaji na kiungo muhimu katika bidhaa nyingi za kielektroniki, hata hivyo dhahabu inabakia kuwa ni bidhaa ambayo ipo siku itakuwa haipatikani kabisa duniani.

Wataalamu wanazungumzia suala la kilele cha madini ya dhahabu, wakati ambapo yamechimbwa kwa wingi zaidi kuliko kipindi chochote kile cha mwaka, huku wengine wakiamini kwamba huenda tayari imefikia hatua ya kumalizika kwa madini hayo.

Uchimbaji wa madini ya dhahabu kwa jumla unasemekana kuwa tani 3,531 mwaka 2019, ikiwa chini kwa asilimia 1 ikilinganishwa na mwaka 2018, kulingana na baraza la usimamizi wa dhahabu duniani, hiyo ilikuwa mara ya kwanza uzalishaji wa dhahabu kupungua tangu mwaka 2008.

Msemaji wa baraza la dhahabu duniani, Hannah Brandstaetter alisema alisema uchimbaji wa madini hayo huenda ukakua kasi ya polepole au ukapungua kidogo miaka ijayo.

Alisema hali hiyo inatokana na kwamba madini hayo yameisha kwenye hifadhi zake na ugunduzi wa hifadhi mpya umekuwa nadra sana hali inayoashiria kwamba kwamba suala la kuwa kilele cha uzalishaji wa dhahabu huenda bado hakijafikiwa.

Hata ikiwa kilele chake kitafikiwa, wataalamu wanasema miaka tu baada ya hatua hiyo, huenda isishuhudie kupungua kwa kiasi kikubwa kwa madini ya dhahabu moja kwa moja, badala yake, kitakachoshuhudiwa ni kupungua taratibu kwa uzalishaji wa madini hayo kwa miongo kadhaa ijayo.

“Uzalishaji wa madini umeshindwa kuongezeka na kuna uwezekano ukapungua, lakini sio kwa haraka mno,” ameongeza Ross Norman wa tovuti ya madini ya MetalsDaily.com.

Kiasi gani cha dhahabu kilichobakia?

Makampuni ya migodi yanakadiria dhahabu iliyosalia chini ya ardhi kwa njia mbili, Hifadhi – dhahabu ambayo inapatikana kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na bei yake wakati huo.

Raslimali – Dhahabu ambayo huenda ikapatikana na kutumika kibiashara baada ya uchunguzi zaidi, au ikiwa itauzwa kwa bei ya juu zaidi

Idadi ya hifadhi ya dhahabu inaweza kuhesabika kwa usahihi zaidi kuliko raslimali, ingawa hili bado sio jukumu rahisi.

Hifadhi ya dhahabu chini ya ardhi kwasasa hivi inakadiriwa kuwa karibu tani 50,000, kulingana na utafiti uliofanywa na idara ya jiolojia ya Marekani.

Ili kuliweka sawa, karibu jumla ya tani 190,000 za dhahabu zimechimbwa ingawa makadirio hayo yanatofautiana. Kulingana na takwimu za makadirio, kuna karibu asilimia 20 ya dhahabu ambazo bado hazijachimbwa.

Aidha teknolojia mpya huenda pia zikawezesha upatikanaji wa madini hayo katika baadhi ya sehemu ambazo sasa hivi hazifikiwi.

Katika baadhi ya sehemu, roboti zimeanza kutumiwa na zinatarajiwa kuendelea kutumika kama hatua moja iliyopigwa kiteknolojia katika uchimbaji wa madini hayo migodini.

Chanzo kikubwa cha madini ya dhahabu katika historia kimekuwa eneo la bonde la Witwatersrand liliopo nchini Afrika Kusini. Witwatersrand, ambapo bonde hilo linakadiriwa kuchangia asilimia 30 ya madini yote ya dhahabu yaliyowahi kupatikana.

Vyanzo vingine vya dhahabu ni mgodi wa Mponeng Afrika Kusini, migodi ya Super Pit na Newmont Boddington iliyopo Australia, mgodi wa Grasberg uliopo Indonesia na ile ya Nevada nchini Marekani.

Hivi sasa China ndio nchi yenye mgodi mkubwa wa dhahabu huku Canada, Urusi, Peru pia nao zikiwa miongoni mwa nchi zinazozalisha madini hayo kwa wingi.

Uchimbaji mkubwa wa madini ya dhahabu unahitaji mtaji mkubwa, mashine kubwa na ya hali ya juu, na wataalamu katika maeneo ya mgodini juu na chini ya ardhi.

Hivi sasa karibu asilimia 60 ya shughuli za uchimbaji wa madini zinafanyika juu ya ardhi, huku asilimia iliyosalia zikifanyika chini ya ardhi.

“Shughuli za uchimbaji madini zinaendelea kuwa ngumu kwasababu migodi mingi ni mikubwa, thamani yake ni ya chini, na pia ni ya zamani sana kama ile ya Afrika Kusini, madini yanakaribia kumalizika,” ameongeza Norman.

Ingawa bei ya dhahabu, ilikuwa juu zaidi mwezi Agosti mwaka 2020, hii haimaanishi kwamba shughuli za uchimbaji dhahabu zinaongezeka.

“Ukiangalia shughuli zinazoendelea, inachukua muda kufanya mabadiliko ya shughuli za uchimabji migodi kwasababu nyinginezo kama vile bei ya bidhaa hiyo”, aliongeza Brandstaetter.

Pia, bei ya juu ya madini hayo iliyorekodiwa, kumetokea wakati wa kipindi cha virusi vya corona na kufanya iwe vigumu kuendesha shughuli za uchimbaji ambapo baadhi ya ama ilifungwa kwa muda au kabisa kama njia moja ya kukabiliana na virusi vya corona.

Kuongeza kwa bei ya bidhaa hiyo kumetokana na janga la corona kwasababu wawekezaji wanachukulia dhahabu kama bidhaa salama wakati wa sintofahamu za hali ya kiuchumi.

Huenda ikawa vigumu kutathmini dhahabu ya chini ya ardhi, lakini sio chanzo cha pekee. Hata hivyo, gharama ya upatikanaji wake na kuisafirisha tena hadi ardhini ziko juu mno ikilinganishwa na thamani ya dhahabu yenyewe.

Hivyo hivyo kuna baadhi ya hifadhi za dhahabu zinazofahamika huko Antaktika ambazo huenda zisiwe na manufaa ya kiuchumi, kwasababu ya hali mbaya ya hewa.

Dhahabu pia inapatikana katika sehemu nyingi za sakafu ya baharini, lakini pia inachukuliwa isiyokuwa na thamani ya kiuchumi.

Tofauti na rasilimali nyingine kama vile mafuta isiyoweza kutumika tena, dhahabu inaweza kuchakatwa tena. Hilo likiwa sawa na kusema, dhahabu haiwezi ikamalizika kabisa hata itakapofikia wakati ikawa haiwezi kuchimbwa tena. Kiasi kikubwa cha dhahabu kinatumika katika bidhaa za kielektroniki ambazo mara nyingi huchukuliwa kama za kutumiwa na mwisho wake ni kutupwa kama vile simu za mkononi. Kiwango cha dhahabu katika utengenezaji wa bidhaa kama simu kina thamani ya pauni kadhaa.