WASHINGTON, Marekani

MCHEZAJI Tennis namba moja duniani Novak Djokovic, amekumbwa na mkasa mkubwa kwenye mechi ya US OPEN baada ya kupiga mpira kwa hasira na kumgonga kwenye koo muokota mipira na kumsababishia maumivu makali.

Kitendo hicho kilimfanya atolewe kwenye mechi hiyo, na kutozwa faini. Kitendo cha mwana tenisi huyo kinatokana na hasira wakati akielekea kupoteza seti alipokuwa nyuma kwa pointi 6-5.

Mwaka 2016 alibamiza racket ya kucheza karibu kumuumiza mwamuzi na kutozwa faini.Pia katika nyakati tofauti alitozwa faini kutokana na utovu wa nidhamu kwa upande wa kina dada Serena Williams,amepata ushindi na kuwashangaza wengi.

Kinda wa Japan Naomi Osaka baada ya kujiweka pembeni kwenye baadhi ya mechi, ili kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani, alirudi ulingoni na kufanikiwa kupata ushindi.Kinda mwingine wa Marekani Coco Gauf alianza vibaya kwa kupoteza mechi yake ya kwanza.