NA MWANDISHI WETU, PEMBA

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein, amesema mgombea Urais aliesimamishwa na CCM chama hicho  hakijakurupuka kwani kimechaguwa mtu mwenye uwezo wa kuwaletea  maendeleo wananchi wa Zanzibar

Alisema Dk, Hussein Ali Mwinyi,  ni kiongozi mahiri aliepimwa na chama hicho kikongwe cha Siasa Tanzania kilichozaliwa na TANU na ASP na kwa

maana hiyo hakikurupuka kumsimamisha na kuwataka Wanaccm na Wananchi kumpa kura kwa wingi, ili aweze kuitekeleza Ilani ya CCM kwa

ajili ya maendeleo ya Wananchi wote.Dk, Shein, aliyaeleza hayo huko katika Kiwanja cha mpira Gando Wilaya

ya Wete Pemba, wakati akimnadi Mgombea huyo wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk, Mwinyi , sambamba na wagombea wote walioteuliwa na Chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba

2020.

Alisema Urais si kazi ya mchezo wala siyakujaribu kama wengine wanavyodhani na mtu pekee anaeweza kuitekeleza kazi hiyo ni mgombea kutoka Chama cha Mapinduzi.

“ Urais sio asali kama kila mtu aonje , ni kazi inayohitaji ujasiri ,ukakamavu na kujiamini , na hivyo kazi hii anaeiweza ni Dk, Hussein Ali Mwinyi kutoka Chama cha Mapinduzi kwani amekubalika katika chama hicho,”alisema.