NA AMEIR KHALID
MIAKA 10 ya uongozi wa Dk. Ali Mohamed Shein ambayo anaitimiza hivi sasa tangu alipoingia madarakani kuongoza Zanzibar kwa vipindi viwili tofauti.
Dk. Shein alianza kuongoza Zanzibar mwaka 2010 kwa kipindi cha miaka mitano, baadaye akaingia tena madarakani katika kipindi cha awamu ya pili mwaka 2015 na hivi sasa ndio anamaliza muda wake wa uongozi kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Hakika tutakumbuka mengi mazuri ambayo Dk. Shein umetufanyia katika kipindi cha uongozi wako, ambao kwa hakika hatuna jinsi lazima uondoke madarakani, la si hivyo basi tungepiga chapuo uendelea kubaki madarakani ili kutupa matamu zaidi.
Kwa hakika kila mwananchi wa Zanzibar ambaye anaona au ambaye haoni lakini anasikia, hatakuwa na hoja yoyote ya kuhoji maendeleo uliotufanyia katika sekta mbali mbali, kwani kila moja inashindana na nyingine kwa utendaji wake.
Hapa leo nitagusia zaidi sekta ya michezo, utamaduni na Sanaa ambazo kwa namna moja au nyingine, umefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuzipa mafanikio kwa ujumla kulinganisha na nyuma tulipotoka.
Kwa upande wa sanaa kuna mafanikio makubwa ambapo Baraza limeweza kupata sheria ya namba 7 ya mwaka 2015 ambayo ni zao la sheria mbili, ambayo imetokana na mgawanyiko wa sheria mbili kabla kulikuwa na sheria ya sensa na filamu na sheria ya sanaa ambazo zimefanyiwa marekebisho mwaka 2015.
Mafanikio mengine ni pamoja na kuwakusanya wasanii wadogo wadogo na kuwaunganisha na vikundi vikubwa kwa ajili ya kupata ujuzi zaidi na kuweza kupata ajira zao.
Vikundi vya sanaa za maonyesho vimeunganishwa kuunda jumuiya ambazo zitazowawezesha kuwa na maamuzi yenye nguvu ,na kuanzisha jumuiya za umoja wa wasanii wa maigizo ,chama cha mashairi pamoja na chama cha wandishi wa vitabu.
Kabla ya kuingia kwa awamu wa saba madarakani, vuguvugu la michezo kwa skuli za sekondari na msingi maarufu tamasha la Elimu Bila Malipo lilipoteza hadhi yake kidogo kulinganishwa na miaka ya nyuma.
Lakini kwa bahati nzuri sana kuingia tu madarakani ulitoa agizo la kurejeshwa tena kwa vuguvugu hilo, na kwa makusudi uliunda idara maalum ya michezo na ndani ya Wizara ya Elimu ili kushughulikia masuala ya michezo na Utamaduni ikiwemo michezo ya Elimu bila Malipo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika kuhakikisha Sanaa inawainua wasanii uliweka miundo mbinu itakayowasaidia wasanii wa Sanaa za maigizo, muziki kwa kupatiwa studio ambayo zitawarahisishia kurikodi kazi zao kama njia ya kuimarisha matarajio ya kuendeleza vipaji vyao hapo Rahaleo.
Malengo ya kuanzishwa kwa studio za Raha leo kuwasaidia wasanii wachanga ,wakati na ambao hawana uwezo wa kwenda kurikodi kwenye vituo binafsi kutokana na gharama kubwa,sambamba na kukuza vipaji vya wasanii wa uimbaji na uimbaji na Filamu.
Kuanzishwa kwa mpango wa SPORT 55 ambao ni mpango maalumu wa kuzipatia skuli 55 vifaa vya michezo kutoka skuli kila wilaya, matengenezo ya viwanja vya michezo pamoja na kuwapatia walimu wa michezo mafunzo yanayohusu uendeshaji, usimamizi na uongozi katika michezo.