BARANI Ulaya ligi Nations league ambayo timu mbalimbali za taifa zilijitupa uwanjani mwishoni mwa wiki,kutafuta nafasi ya kuongoza kwenye makundi yao.

Uingerza ilipata ushindi mwembamba ugenini dhidi ya Iceland, ushindi ambao kwa kiasi fulani unaweza kuonekana kama ni wa bahati kwani hadi dakika 90 za kawaida, timu hizo zilikuwa bado hazijafungana.

Raheem Sterling alifunga goli katika dakika za majeruhi na kuipatia ushindi huo. Ujerumani ikiwa ugenini walibanwa mbavu bila kutarajia na timu ya Uswisi, na kutoka suluhu ya goli moja kwa moja.

Ufaransa  pia walibahatika kupata ushindi mwembamba wa goli moja kwa bila, goli lililofungwa na mchezaji Kylian Mbappe.