ANKARA,UTURUKI

RAIS  wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameutaka Umoja wa Ulaya katika mvutano wa kuwania uchimbaji wa gesi na Ugiriki, kuchukua msimamo wa kutokuwa na upande.

Ofisi ya Rais wa Uturuki ilisema, katika suala hili litakuwa mtihani mkubwa kwa Umoja wa Ulaya kuhusiana na haki.

Umoja wa Ulaya na mataifa wanachama wa Umoja huo wanapaswa kusimama katika njia ya haki na usawa, bila kuchukua upande na kuwa wakweli, katika suala la kanda hiyo ,na kutambua wajibu wao hususan katika eneo la mashariki mwa bahari ya Mediterania.

Ugiriki na Uturuki kila moja inadai umiliki wa eneo la maji la mashariki mwa Mediterania, ambalo linafikiriwa kuwa lina utajiri mkubwa wa mafuta na gesi.