NA ZAINAB ATUPAE
FAINALI ya kutafuta bingwa wa mashindano ya ‘Sunday Talent Veteran Ndondo cup’, inatarajiwa kupigwa leo katika uwanja wa Mchangani Mjini Unguja.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili huko Mnazi Mmoja Mratibu wa mashindano hayo Abdalla Thabit.
Alisema fainali hiyo itapigwa kati ya Real Zanzibar na timu ya Bububu majira ya saa 10:00 jioni.
Alisema bingwa katika mashindano hayo atapata mbuzi wawili wenye thamani shilingi 300,000 na mshindi wa pili atapewa mbuzi mmoja mwenye thamani ya 150,000.
Alisema msimu huu hakutakuwa na zawadi kubwa kwani mashindano hayakupata mdhamini,licha ya kuhangaikia kutafuta mdhamini.
Alisema malengo ya mashindano hayo ni kuwashajihisha wazee kufanya mazoezi mara kwa mara,ili kujikinga na maradhi,ikiwemo kisukari,presha na maradhi ya baridi, ambayo yameonekana kuwa tatizo kubwa kwa jamii.