NA TATU MAKAME

SAIDI Nasibu Ali (28) mkaazi wa Bububu Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja, amepelekwa Chuo cha Mafunzo Wilaya ya Mjini baada ya kushindwa kujidhamini kwa shilingi milioni 1,000,000.

Mshitakiwa huyo alipelekwa huko baada ya kukabiliwa na kosa la kujaribu kumnajisi mtoto wa kiume aliyechini ya uangalizi wa wazazi wake.

Masharti hayo ni pamoja wadhamini watatu wenye kusaini bondi ya kiasi kama hicho pamoja na barua za sheha na vitambulisho vya Mzanzibar mkaazi masharti ambayo yalimshinda.

Akisoma kosa la mshitakiwa huyo Mwendesha Mashitaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Issa Salim Mbele ya Hakimu Saaduni Bakari Hassan wa Mkoa Mkoa wa Vuga alisema kosa hilo ni kinyume na sheria.

Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mnamo Julai 15, 2019 majira ya saa 12:00 Bububu Mkoa wa Mjini Magharini Unguja, mshitakiwa huyo alitenda makosa mawili ikiwemo kosa la kutaka kujaribu kumlawiti mtoto wa miaka tisa aliyechini ya uangalizi wa wazazi wake kinyume na kifungu cha 115 (2) cha sheria namba 6 ya mwaka 2018.

Kosa la pili ni shambulio la aibu kinyume na kifungu cha 135 cha sheria namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar, ambapo ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo siku hiyo alimchukua mtoto huyo na kumpeleka mbali na nyumbani kwao kisha kuipandisha suruwali yake aliyokuwa ameivaa na kumsugulia uume wake sehemu za siri jambo ambalo ni kosa kisheria.

Hata hivyo Mshitakiwa huyo alipewa nafasi ya kujidhamini masharti ambayo yalimshinda ndipo alipoamriwa aende rumande hadi Septemba 16 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena mahakamani hapo.