NAIROBI, Kenya

KLABU ya Gor Mahia ya Kenya imeendelea na tatizo la kupoteza wachezaji wake, wanaohamia katika klabu nyingine.

Hali hii imewafanya baadhi ya wapenzi wa klabu hiyo kukata tamaa kama tiumu yao itarudi katika ubora wake wa soka nchini Kenya kama ilivyokuwa kwenye miaka ya 70 na 80.

 Ikiwa ni katika hali ambayo imeonekana kama ni kuwatia moyo mashabiki, ofsa mmoja wa klabu alitoa maneno amabyo yaliwashangaza wengi, kwa kusema kuwa  endapo wanawake wa eneo la Luo wataendelea kuzaa watoto wa kiume, basi timu hiyo itaendelea kuwepo na itasonga mbele.

Lakini amesisitiza umuhimu wa kuheshimu kanuni za klabu bila kujali mchezaji ni nani.