KÓPAVOGUR, Iceland.
WACHEZAJI vijana wa timu ya taifa ya England Phil Foden na Mason Greenwood hawakusafiri na timu kwenda Denmark, baada ya picha zilizoibuka za wawili hao kudaiwa kuingiza wanawake kwenye hoteli ya timu huko Iceland.
Wawili hao waliitwa kwenye timu ya wakubwa iliyoishinda Iceland Jumamosi.Wachezaji wamepewa miongozo madhubuti kuhakikisha wanakuwa salama na Covid – 19, na picha – zilizochapishwa na duka la Icelandic outlet DV, zinawaonyesha Foden na Greenwood wamepuuza hatua hizo.
Kitendo hicho cha kuingiza wanawake katika kambi ni ukiukwaji wa sheria na katiba za FA kwa wachezaji wakati wakiwa katika jukumu la timu ya taifa.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Foden na Greenwood walionekana wamevalia fulana mpya za mazoezi za England na wachezaji hao hivi sasa suala lao linajadiliwa na uongozi.
Msichana mwingine alidai kuwa amewajulisha nyota wa England kuwa picha hizo zilikuwa zinasambazwa na ujumbe wa Snapchat, lakini ‘hawajazifungua’.