LONDON, England

KOCHA Pep Guardiola, 49, amesema atatia saini mkataba mpya kuendelea kuifundisha timu  ya Manchester City, iwapo atahisi anastahiki kufanya hivyo.

Mkataba wa sasa kati ya mkufunzi huyo raia wa Uhispania na Man-City unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, na timu hiyo ipo kumuona  Guardiola akirefusha mkataba wake Etihad.

Guardiola alianza msimu wake wa tano akiwa na timu hiyo  jana Septemba 21 kwa kuvaana na Wolves katika mchezo wa  Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) katika uwanja wa Molineux.

Hiki ndicho kipindi kirefu zaidi kwa Guardiola kuhudumu katika kikosi kimoja baada ya kuifundisha Barcelona mwaka 2008-2012 na Bayern Munich 2013-2016.

 Kwa mujibu wa Guardiola, hakuna yeyote kati ya Mwenyekiti Khaldoon Al Mubarak au Ofisa Mkuu Mtendaji Ferran Soriano ambaye amewahi kumzungumzia kuhusu mkataba mpya.

Ingawa anahisi kwamba matarajio kutoka kwake ni ya kiwango cha juu hasa baada ya kusuasua kwao muhula uliopita ambao ulishuhudia pengo la pointi 18 mbelea mabingwa Liverpool.