LONDON, England
MENEJA wa Manchester City, Josep ‘Pep’ Guardiola, anaongoza kwenye orodha ya mameneja wanaolipwa mshahara mkubwa kwa wiki katika Ligi Kuu ya England.

Guardiola ambaye aliajiriwa Etihad mamo mwaka 2016 akitokea kwa mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, imetajwa kulipwa mshahara mkubwa wa pauni 417,500 kwa wiki.

Meneja wa mabingwa wa England, Jurgen Klopp, anafuatia kwenye orodha hiyo akilipwa mshahara wa pauni 313,500 kwa wiki.

Orodha ya mishahara ya baadhi ya mameneja wanaofundisha England walioingia 10 bora ni pamoja na Jose Mourinho (313,000), Carlo Ancelotti (230,000), Frank Lampard (166,850), na Marcelo Bielsa (166,660).

Wengine ni Ole Gunnar Solskjaer (160,000), Bendan Rodgers (105,000), Mikel Arteta ( 105,000) na Roy Hodgson (93,750). (Goal).