NAIROBI,KENYA

RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya ametaka hatua za haraka na madhubuti zichukuliwe ili kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika.

Rais Kenyatta alisema hayo kwenye uzinduzi wa tawi la Afrika la Kituo cha Kimataifa cha Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi.

Alisema changamoto hizo zilizidishwa na janga la COVID-19, ambalo limevuruga uchumi wa dunia, ingawa janga hilo halijahusiana moja kwa moja na mabadiliko ya tabianchi, lakini matumizi ya rasilimali katika kupambana na janga hilo na kupunguza athari zake kwa uchumi, bila shaka yamepunguza kile kinachopatikana kushughulikia mabadiliko ya tabianchi.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo, uvamizi wa nzige wa jangwani nchini Kenya na kwenye nchi nyengine za Afrika Mashariki umeathiri vibaya maisha ya wakulima, na kuleta tishio dhidi ya usalama wa chakula ambalo halijawahi kushuhudiwa.