MILAN, Itali

MSHAMBULIAJI wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic amethibitika kupata maambukizi ya virusi vya Corona na sasa atawekwa karantini wakati huu akilazimika kufuata taratibu za matibabu ya virusi hivyo.

Zlatan ndio mchezaji pekee katika orodha ya AC Milan aliyekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona, wafanyakazi wa timu ya AC Milan wakiwemo wa benchi la ufundi wote wako salama.

Taarifa kutoka AC Milan inaeleza Zlatan amepata maambukizi ya COVID-19 wakati wa mzunguuko wa pili wa vipimo.