Mwanasiasa mkongwe na mfanyabiashara maarufu Salim Hassan Abdullah Turky, afariki dunia usiku huu akiwa hospitali ya Tasakhta global chanzo cha kifo chake inadaiwa kua aliugua hafla.

Salim Turky alikuwa mfanyabiashara maarufu Zanzibar na mbunge wa jimbo la Mpendae tangu 2010, alizaliwa February 11, 1963. Mpaka anafariki alikuwa mwenyekiti wa makampuni ya Turky ambapo chini yake yalikuwa makampuni 12 yanayoendesha biashara zake Tanzania Bara, Zanzibar na visiwa vya Comoro.

Baadhi ya makampuni hayo yanajumuisha hoteli ya Golden Tulip, hospitali kubwa ya Tasakhtaa Zanzibar, pia ilijihusisha na biashara ya cement, Nitak communications, vyakula, mafuta,gesi na meli ya Zan fast ferries
#CCM #Zanzibar