TEHRAN, Iran

IRAN imesema imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya mpiganaji mieleka Navid Afkari aliyekutwa na hatia ya kumuua mwanamme mmoja wakati wa maandamano dhidi ya serikali yaliyofanyika mwaka 2018, hatua iliyoibua shutuma kali na mshtuko kutoka kwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa – IOC.

 Mahakama nchini Iran imesema Afkari alipatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia kwa kumchoma kisu Hossein Torkman, Agosti 2 mwaka 2018.

IOC imesema imeshtushwa na kutekelezwa kwa hukumu hiyo, na kwamba inasikitisha kuwa wito uliotolewa na wanariadha kote duniani na mashirika ya kimataifa imeshindwa kuzuia hatua hiyo.