YERUSALEMU, ISRAEL

UMOJA wa Mataifa umetangaza kuwa utawala wa Israel umebomoa zaidi ya nyumba mia tano za raia wa Palestina.

Ripoti iliyotolewa na Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) ilisema kuwa,tangu mwanzoni mwa mwaka huu utawala wa Israel umebomoa nyumba 506 za Wapalestina.

OCHA ilisema 134 kati ya nyumba hizo zilibolewa katika Quds inayokaliwa kwa mabavu.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliongeza kuwa wiki mbili zilizopita peke yake Israel ilibomoa nyumba 22 za raia wa Palestina.

Ocha ilsema baadhi ya nyumba hizo zilibomolewa kwa kisingizio kwamba hazikuwa na vibali na nyengine kwa kuwekewa kodi kubwa kupita kiasi.

Wakati huo huo Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa,Jamie McGoldrick alisema Israel ilizidisha bomoa bomoa ya nyumba za Wapalestina katika miezi ya karibuni sambamba na maambukizi ya virusi vya corona.

Utawala haramu wa Israel umekuwa ukiboa nyumba na maeneo ya kihistoria ya Palestina kwa shabaha ya kubadilisha muundo na jiografia ya maeneo hayo na kuyapa sura ya kiyahudi kwa kujenga vitongoji vya walowezi wa kizayuni katika maeneo hayo.