YERUSALEMU, ISRAEL

ISRAEL imetangaza kuwa itazifunga tena shughuli zote nchini humo kwa muda wa wiki tatu, katika juhudi za kudhibiti wimbi jipya la maambukizi ya virusi vya corona linaloshika kasi.

Israel inakuwa nchi ya kwanza yenye uchumi ulioendelea kuchukuwa hatua kali kama hizo kushughulikia wimbi la pili la maambukizi ya COVID-19.

Awali nchi hiyo ilisifiwa kwa namna ilivyoweza kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo uliporipuka nchini humo mwezi Machi, lakini wakati huu ni ya pili duniani baada ya Bahrain kuwa na visa vingi kwa kuzingatia idadi ya jumla ya wakaazi wake.

Alipoyatangaza masharti hayo mapya kwa njia ya televisheni Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema upo uwezekano kwa muda wa masharti hayo kurefushwa.

Alisema lengo ni kusimamisha kasi ya maambukizi ambayo hivi sasa ilipindukia visa 4000 kwa siku.