YAMOUSSOUKRO, IVORY COAST

SERIKALI ya Ivory Coast ina mpango wa kuwachia huru washirika wa kiongozi wa upinzani nchini humo Guillaume Soro ikionekana kama shabaha ya kupunguza mvutano wa ndani wa taifa hilo katika kipindi hiki likijiandaa na uchaguzi.

Msemaji wa Serikali alisema waliwashikilia watu hao kwa miezi kadhaa sasa.

Watu hao wa karibu na Soro,ambao wanajumuisha wabunge watano walikuwa wakishikiliwa bila kupandishwa kizimbani tangu wakamatwe Desemba kutokana na kile ambacho kinaelezwa kuhusika na jaribio la mapinduzi ambalo linaongozwa na Soro mwenyewe ambae kwa hivi sasa anaishi uhamishoni Paris.

Uamuzi wa Rais Alassane Ouattara kuwania tena muhula wa tatu, kufuatia kifo cha ghafla cha mtu aliyetajwa kuwa mrithi wake Julai ulisababisha vurugu za maandamano.

Upinzani unashinikiza machafuko zaidi kuelekea uchaguzi wa Oktoba 31.