TOKYO,JAPAN

SERIKALI ya Japani imeandaa rasimu ya miongozo ya muda juu ya chanjo za virusi vya corona.

Rasimu hiyo inaonyesha kwamba wataalamu wa tiba na wazee watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupatiwa.

Ilisema wahudumu wa afya wapo katika hatari kubwa ya maambukizi na wazee wana uwezekano wa kupata dalili kali za virusi hivyo.

Rasimu hiyo inasema majadiliano zaidi yatafanyika kuhusiana na kwa kiasi gani wajawazito na watoa huduma kwa wazee wanapaswa kupewa kipaumbele.

Kadhalika Rasimu hiyo inasema Serikali kuu itachukua hatua za kuhakikisha kuwa mamlaka za maeneo hazitawajibika kifedha kwa ajili ya chanjo hizo.

Inasema Serikali itatekeleza hatua za utoaji msaada kwa madhara ya kiafya ambayo yanaweza kusababishwa na chanjo hizo.

Rasimu hiyo inaongeza kuwa serikali pia itaandaa mipango ya kisheria ya kulipa fidia makampuni ya kutengeneza dawa kwa hasara yoyote inayoweza kuwapata kutokana na madhara hayo.