CAIRO,MISRI

JESHI la Misri limetangaza kuwa limeua magaidi zaidi ya 70 wenye muungamano na genge la kigaidi la Daesh (ISIS) katika operesheni za vikosi vya usalama vya nchi hiyo katika Mkoa wa Sinai Kaskazini.

Taarifa ya jeshi hilo ilisema magaidi 73 waliuawa katika operesheni kadhaa ya vikosi vya Serikali dhidi ya ngome na maficho ya magaidi hao katika Peninsula ya Sinai, baina ya Julai 22 na Agost.

Taarifa hiyo bila kutoa maelezo ya kina iliongeza kuwa,magaidi wengine wanne waliuawa huku askari saba wa Misri pia wakiuwa ma kujeruhiwa katika operesheni hizo.

Mapigano huwa yanatokea mara kwa mara baina ya magenge ya kigaidi na jeshi la Misri katika Mkoa wa Sinai ulioko kaskazini mwa nchi hiyo na katika baadhi ya maeneo mengine ya Misri.

Wanajeshi wanane wa Misri waliuawa katika mripuko wa bomu uliotokea katika njia ulipokuwa ukipita msafara wa wanajeshi hao katika mkoa wa Sinai ya Kaskazini nchini humo.

Aidha wanajeshi wengine watatu wa jeshi la Misri waliuawa na wanne walijeruhiwa katika mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na magaidi katika mkoa huo.