NA MWANDISHI WETU

WANANCHI Watanzania wametakiwa kutofanya majaribio ya kuwachagua viongozi wasiokuwa na uwezo wa kuwatumikia, kwani hakuna hata robo ya wagombea waliosimishwa kuwania nafasi ya Urais wataokifikia Chama cha Mapinduzi.

Mgombea wa CCM nafasi ya Urais, John Pombe Magufuli aliyasema hayo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika huko Chato Mkoa wa Mwanza.

Magufuli alisema Chama cha Mapinduzi kimekuwa na uzoefu wa kuiongoza Tanzania na lazima wananchi wakatae kufanya majaribio kwa wagombea wengine na badaya yake waendelee kuimamini CCM kwani ina mambo mengi ya maendeleo inayotaka kuyatekeleza ndani ya miaka mitano ijayo.

“Mimi naijua Tanzania yote, nawajua watanzania wanataka nini Urais unakazi kubwa msijaribu  kuongoza kuna gharama kubwa nimekumbana na changamoto nyingi za kiuchumi za kiusalama na kijamii msijaribu  watu wengine wanaogombea wote hao hata robo hayupo mwenye uwezo wa kuyafikia tulipo sasa” alisema Magufuli.

Alisema kuna baadhi ya wagombea wametangaza watawapa chakula Watanzania, lakini jambo la kushangaza ndani ya familia zao zinashindwa kula vizuri huku wengi wakidai kuwa wakishinda watanzania hawatakuwa na kazi ya kujiletea maendeleo, wakati vitabu vya dini vinaelekeza asiefanyakazi asile.