ATHENS,UGIRIKI

MOTO ulizuka katika kambi yenye wakimbizi wengi nchini Ugiriki ya Moria katika kisiwa cha Lesbos.

Maofisa wa Idara ya zima moto walisema sababu za kuzuka kwa moto huo hazijafahamika, ambapo moto uliwaka ndani na nje ya kambi hiyo.

Ofisa wa polisi alisema kuwa wahamiaji wanaondolewa na kupelekwa katika sehemu salama.

Watu walionekana wakiondoka katika kambi hiyo, wakibeba mizigo yao mikononi.

Kiasi ya wazima moto 28 wakiwa na magari tisa,wakisaidiwa na watu waliojitolea,wanapambana kuuzima moto huo.

Kambi ya Moria, ambayo inawahifadhi zaidi ya watu 12,000 zaidi ya mara nne ya uwezo wake,mara nyingi ilikosolewa na makundi ya kutoa misaada kutokana na mazingira mabovu ya kuishi.