ZASPOTI
NYOTA wa zamani wa kimataifa wa Rwanda, Pascal Rurangirwa Karekezi amestaafu mashindano ya mpira wa kikapu akiwa na umri wa miaka 26.
Aliweka habari za kustaafu kwake katika barua ya hisia ya ‘Instagram’ juzi.


Karekezi alikuwa sehemu ya timu ya mpira wa kikapu ya Patriots iliyoshinda taji la Ligi ya Kitaifa ya BK ya msimu wa 2018/29 mnamo Septemba iliyopita baada ya kurudi mchezoni ikitoka nyuma ya 3-1 na kuifunga Rwanda Energy Group 4-3 katika fainali za michezo ya mchujo.
“Mpira wa kikapu ulikuwa kila kitu kwangu na nilipata vitu vingi kupitia huo mchezo, sikufikiria siku itakuja ambapo nitatangaza kustaafu. Lakini, huu ni wakati huo na niko tayari kuendelea mbele”, alisema, Karekezi.


“Ninamshukuru kila mtu ambaye aliniunga mkono wakati wa safari hii [ngumu] ya kuzichezea klabu tofauti za hapa Rwanda na timu ya taifa”, akaongeza.
Nyota huyo wa zamani wa Espoir hakueleza sababu za kustaafu kwake, lakini, hakuwa katika kiwango cha juu katika miaka miwili iliyopita.


Wakati Karekezi ana kazi nzuri ya kupendeza katika mpira wa kikapu wa kimataifa, atakumbukwa pia kama mwenye kipaji ambaye hakufikia uwezo wake kamili kwani alishindwa kung’ara katika kiwango cha juu licha ya kupokea wito wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17.


Aliiongoza timu ya taifa ya chini ya umri wa miaka 18 kupitia Mashindano ya 2010 ya FIBA Afrika chini ya miaka 18 ambapo wenyeji Rwanda walimaliza katika nafasi ya sita kati ya timu 11 kwenye mashindano hayo.
Ngazi ya klabu, Karekezi pia alionekana akiwa na timu za mpira wa kikapu za APR na United Generation. (Rwanda News).