NAIROBI,KENYA
KENYA kupitia Wizara ya EAC imeanzisha mazungumzo ya kidiplomasia ili kutatua msuguano wa mizigo katika mipaka ya Busia na Malaba.
Hatua hiyo inafuatia ripoti kwamba Serikali ya Uganda ilitoa maagizo mapya ya kuwataka madereva wote wa malori wanaoingia nchini kupitia Busia na Malaba kufanya vipimo vyengine vya Covid-19 bila kujali kuwa washafanya vipimo vyengine Kenya.
Serikali ya Uganda ilibatilisha uamuzi wake wa upimaji wa bure wa madereva wa malori na uwezeshaji wa usafirishaji wa bidhaa.
Maendeleo hayo mapya yalisababisha msongamano wa trafiki kwenye vituo vya mpaka, na foleni huko Malaba ina urefu wa kilomita 20-30 kuingia Kenya, wakati madereva wanasubiri kibali.
Malori na madereva wa Kenya wanachukua asilimia 87 ya harakati za usafirishaji kati ya Mombasa na bara.
Kulingana na makubaliano ya hapo awali kati ya nchi wanachama wa EAC, waendeshaji malori wote walitakiwa kufanya vipimo vya Covid-19 katika nchi yao ya asili kabla ya kuanza kwa safari yao.
“Huenda kuna kitu kilitokea kuhamisha Uganda katika nafasi hiyo. Tutaweza kujua kwa wakati unaofaa ni mambo gani na nina hakika kutakuwa na majadiliano na mazungumzo, ”CAS wa Afya Rashid Aman alisema.
Uganda iliamua kutoza vipimo baada ya Kenya kushindwa kutekeleza zoezi hilo kwa ufanisi, na hivyo kuzidiwa na madereva wa Kenya wanaotafuta huduma kutoka upande wa Uganda.
CAS ilibaini kuwa suala hilo lisiposhughulikiwa kwa dharura linaweza kusababisha gharama kubwa za biashara.
Nairobi inaendelea kuongoza kwa idadi ya kesi mpya baada ya kusajili maambukizo mengine 96, ikifuatiwa na Mombasa na 21, Kiambu 11, Busia kumi , Uasin Gishu na Laikipia tisa, Taita Taveta na Narok wanane, Machakos na Nakuru saba, Kilifi na Lamu sita kila moja, Kajiado nne, Bomet mbili, Bungoma, Kericho, Kwale, Migori, Murang’a, Nyeri, Pokot Magharibi na Meru walirikodi kesi moja kila mmoja.