NA MARYAM SALUM, PEMBA

MTUHUMIWA Mkubwa Abdalla Mjaka miaka 20, anaekabiliwa na tuhuma za kutorosha na kubaka kwa kikundi, mtoto mwenye miaka 16, imelazimika kesi yao kuahirishwa na mahakama ya Mkoa Chake Chake, kutokana na kuwepo  kwenye mitihani.

Wakati mtuhumiwa mwenzake namba mbili Azizi Idrisa Abdalla mwenyemiaka 23, akiwa ametinga kizimbani akisubiri taratibu za mahakama,ndipo Mwendesha mashitaka Mohamed Ali Juma alipodai kuwa, shauri hilolipo kwa kusikilizwa ingawa mtuhumiwa namba moja hakufika mahakamani kutokana na kuwa yupo kwenye mitihani.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, watuhumiwa hao walitenda makosa manne kwa nyakati tofauti.

Kosa la kwanza kwa pamoja siku na tarehe isiyofahamika Januari mwakahuu majira ya saa 12:00 jioni, Vitongoji Chake Chake, bila halali na bila ridhaa ya mzazi wake, walimtorosha mtoto mwenye miaka 16, kutoka nyumbani kwao Vitongoji na kwenda nae Vitongoji makaani.

Kosa la pili kwa watuhumiwa hao, walilitenda Aprili mwaka huu saa 1:45usiku Vitongoji, bila halali na bila ridhaa ya mzazi wa mtoto walimtorosha, jambo ambalo ni kosa kinyume na kifungu cha 113 (a) cha Sheria namba 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.

Kosa la tatu kwa watuhumiwa hao, walilitenda siku ya tarehe isiyofahamika mwezi Januari mwaka huu, majira ya saa 11:45 jioni eneo la Vitongoji, ambapo wote kwa pamoja walimbaka mtoto mwenye miaka 16,jambo ambalo ni kosa kisheria.

Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 108 (1) (2) (e) na 110(1) (2) sheria ya adhabu namba 6 ya mwaka 2018.

Kosa la nne kwa watuhumiwa hao ilidaiwa kulifanya tukio hilo siku na tarehe isiyojulikana mwezi Febuari mwaka huu majira ya saa 1:30 usiku Vitongoji Mchangani wote kwa pamoja walimbaka mtoto huyo, jambo ambalo ni kosa kisheria.

Kubaka kwa kikundi ni kosa kinyume na kufungu cha 108 (1) (2) (e) na kifungu cha 110 (1) (2) vya sheria namba 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.