NA ZAINAB ATUPAE
TIMU ya Kiembe Samaki imefanikiwa kuendelea na mashindano ya Coco Sport Ndondo baada ya timu hiyo kutofungana dhidi ya Mazombi.
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Kiembe Samaki Majira ya saa 10:00 jioni ambao ulikuwa na ushindani kwa timu hizo.
Hadi timu zinakwenda Mapumziko hakuna aliyefanikiwa kuzifumua vyavu za mwenzake.
Kurudi uwanjani kumalizia mchezo huo timu ziliingia na kasi kubwa ambapo kila timu ilifanya mabadiliko kurekebisha kikosi chake,lakini hadi dakika 90 zinamalizika hakuna aliyefanikiwa kupata bao kwa mwenzake.
Kwa matokeo hayo timu ya Kieme Samaki ilifanikiwa kuendelea na mashindano hayo kwa faida ya bao la ugenini, baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa kwanza.