NA CHRISTINA MWAGALA
KOCHA wa timu ya mpira wa miguu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC Habibu Kondo, amesema kikosi chake kipo tayari kumenyana na timu ya Mbeya City siku ya Jumatatu katika mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2020/ 2021 katika dimba la uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kumalizika mazoezi yao leo, kocha Habibu amesema, muendelezo wa mazoezi hayo yatatoa nafasi ya kurekebisha mapungufu yanayojitokeza ili kukiweka sawa kikosi hicho kabla ya kukutana na wapinzani wao.
Kocha huyo Mtanzania ameeleza kuwa timu hiyo kwa sasa wachezaji wanabidii na wana imani katika msimu huu, itapata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kuchukua ubingwa.
Ameongeza kuwa msimu huu timu hiyo imefanyiwa maboresho makubwa ikiwemo kurekebisha kasoro ambazo zilijitokeza msimu uliopita na kwamba mashabiki wategemee kupata burudani.