NA MWAJUMA JUMA

SERIKALI imeshauriwa kuwashajihisha vijana kuendelea kucheza mchezo wa mpira wa kikapu ili waendelee kucheza mchezo pindi wanapomaliza masomo yao.

Ushauri huo umetolewa na kocha wa timu ya Clickers ya mpira wa Kikapu alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya vijana wa kisiwa cha Pemba kutojihusisha na michezo.

Alisema Pemba kuna vijana wengi ambao hushiriki michezo wakiwa skuli lakini wanapomaliza masomo yao, huacha kuendelea na mchzo huo kutokana na hali za maisha.

Alitoa mfano katika mchezo wa mpira wa kikapu kwa takriban miaka sita, skuli za sekondari na msingi wamekuwa mabingwa lakini wanafanya hivyo kwa kuwa wapo skulini na wakimaliza wanakaa pembeni kufanya shughuli zao za kimaisha.

Hivyo aliiomba serikali kuwatia nguvu vijana hao kwa kuwatafutia wadhamini hasa kwa vile mchezo huo ni miongoni mwa michezo inaypendwa sana kisiwani humo.